utangulizi
Historia Fupi ya Kanisa
Usharika wa Kimara ulianzishwa mwaka 1972 kama mtaa mdogo chini ya Usharika wa Ubungo.Ibada za kwanza zilifanyika nyumbani kwa Mzee Onesmo Ngowi aliyetoa chumba kwa ajili ya ibada.Mwaka 1976, eneo la kujenga kanisa lilipatikana, na idadi ya waumini ikaongezeka kwa haraka.Hatimaye, mwaka 1983, mtaa huu ukapewa hadhi ya kuwa Usharika kamili.
Ukuaji wa KKKT Usharika wa Kimara
Ukuaji wa Usharika wa Kimara umechangia kuanzishwa kwa Sharika mbalimbali kama Msewe, Temboni, Mbezi Luisi, King’ong’o, na Mavurunza. Kuanzia mwaka 2009, huduma za kiroho chini ya Mchungaji Willbroad Mastai zilichangia ongezeko kubwa la waumini kwa wastani wa asilimia 18 kila mwaka. Idadi ya waumini iliongezeka kutoka 2,354 mwaka 2011 hadi 6,467 mwaka 2022. Huduma za Neno la Mungu, Maombi na Maombezi zimekuwa msingi wa mafanikio haya.
Dira Yetu
Kuwa kiongozi katika kutangaza Injili ya Yesu Kristo kwa watu wote na mataifa yote duniani.
Malengo
Kufundisha na kuhubiri neno la Mungu na injili ya Yesu Kristo kwa watu wote. Hii ni pamoja na kuendelea kugusa maisha ya wahitaji na kutoa huduma kwa jamii, tukiyaishi mafundisho na upendo wa Yesu Kristo.