kipaimara
Kipaimara
Huduma ya Kipaimara ni huduma maalum inayotolewa kwa lengo la kuwaimarisha na kuwajenga watoto katika imani ya Kikristo ili kuimarisha maisha yao ya kiroho na kimwili.Mafundisho haya huwasaidia watoto kuelewa uwezo na ukuu wa Mungu, kujiandaa kuwa Wakristo imara wanaomtumikia Mungu, kuutangaza ukuu wake, na kumshuhudia Kristo katika maisha yao ya kila siku.
Utaratibu wa Mafundisho ya Kipaimara
Mafundisho ya Kipaimara hutolewa kwa muda wa miaka miwili kwa watoto wenye umri kati ya miaka 11-12. Mafundisho hufanyika mara mbili kwa wiki kama ifuatavyo:- Alhamisi: Kuanzia saa 11:00 jioni hadi 12:00 jioni.
- Jumamosi: Kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi 5:00 asubuhi.
- Usajili wa watoto wanaojiunga na Kipaimara.
- Utoaji wa mafundisho kulingana na muongozo wa Kanisa.
- Kuwajaribu wanafunzi ili kuthibitisha uelewa wao kabla ya kupokea Kipaimara.
Darasa la Nikodemu
Darasa la Nikodemu ni huduma maalum ya mafundisho ya Kipaimara na Ubatizo kwa:- Watoto wenye umri wa miaka 15 au zaidi.
- Watu wazima wanaohitaji mafundisho ya Kipaimara na Ubatizo.
Utaratibu wa Darasa la Nikodemu
Utaratibu wa Kujiunga
Tangazo la kujiunga na Darasa la Nikodemu hutolewa kupitia:- Matangazo ya Usharika
- Ofisi ya Mwinjilisti wa Usharika
Huduma hii inalenga kuwasaidia wanafunzi kufikia kiwango cha uelewa wa imani ya Kikristo kwa mujibu wa mafundisho ya Kanisa la KKKT.
Karibuni nyote kwa ajili ya kujifunza, kujengwa kiroho, na kuimarishwa katika imani ya Kikristo.