ndoa
Ndoa
Ibada ya ndoa katika Usharika wa KKKT Kimara hufanyika kila siku ya Jumamosi kuanzia saa 9:00 alasiri. Hata hivyo, kipindi cha Kwaresima, ibada hii haitolewi isipokuwa kwa kibali maalum.
Usharika pia hutoa huduma ya ndoa za pamoja kwa wanandoa waliokaa muda mrefu bila kubariki ndoa zao au kwa wale walio na ndoa za kiserikali na wanapenda kufunga ndoa ya kanisani. Ndoa hizi hufungwa pale panapobainika kuwa na mahitaji.
Taratibu za Kufunga Ndoa
- Kuandikisha Ndoa: Wanandoa wanatakiwa kuandikisha ndoa zao miezi mitatu (3) kabla ya tarehe ya kufunga ndoa.
- Mafundisho ya Ndoa: Mafundisho ya ndoa yanaandaliwa na Dayosisi kwa mujibu wa mwongozo wa KKKT.
Kwa taarifa zaidi au ushauri wa kina kuhusu huduma hii, tafadhali wasiliana na ofisi ya Usharika wa KKKT Kimara.
Ndoa ni zawadi takatifu kutoka kwa Mungu - Basi na tuifunge kwa heshima na ibada.