ibada ya jumapili
Ibada ya Jumapili
Ibada ya Jumapili katika Usharika wa KKKT Kimara ni moja na hutolewa kwa lugha ya Kiswahili.Ibada huanza saa 1:00 asubuhi na huambatana na huduma mbalimbali kama ifuatavyo:-
- Ubatizo
- Huduma ya ubatizo wa watoto na watu wazima hutolewa kwa mujibu wa ratiba ya kanisa.
- Sakramenti ya meza ya Bwana
- Hufanyika mara moja kwa mwezi.
- Huduma hii pia hutolewa kwa wagonjwa hospitalini au nyumbani kwa utaratibu maalum.
- Fungu la Kumi
- Hutolewa kila Jumapili ya kwanza ya mwezi kama sehemu ya ibada.
- Ibada ya kusifu na kuabudu
- Hufanyika kwa utaratibu uliowekwa na Usharika kwa lengo la kukuza moyo wa ibada na sifa.
- Ibada ya mkesha wa maombi
- Hufanyika kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi kwa ajili ya kuomba na kuombeana.
- Ibada ya Ndoa
- Hufanyika kwa utaratibu unaoelekezwa na Usharika.
- Kipindi cha Kwaresima, ibada hii haitolewi isipokuwa kwa kibali maalum.
- Usharika pia hutoa huduma ya ndoa za pamoja kwa washarika waliokaa muda mrefu bila kubariki ndoa au waliokuwa na ndoa za serikali. Huduma hii hutolewa pale panapokuwa na mahitaji.