shule ya jumapili
Shule ya Jumapili
Usharika wa KKKT Kimara unatoa huduma ya Ibada ya Watoto inayofanyika kila Jumapili wakati wa Ibada ya Kwanza. Huduma hii hutolewa kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili kuhakikisha watoto wote wanapata nafasi ya kuelewa mafundisho ya Neno la Mungu.
Watoto hugawanywa katika makundi kulingana na umri wao ili mafundisho yawe ya kina na yenye kujenga uelewa wa Neno la Mungu kwa hatua zao za kiukuaji. Ibada hii inaambatana na:
- Mafundisho ya Neno la Mungu.
- Ushiriki wa watoto katika vikundi mbalimbali kama kwaya, maigizo, ngonjera,mashairi, jiving na shughuli nyingine za kuburudisha na kujenga vipawa.
Huduma hii inalenga kuwajenga watoto kiroho na kimwili, kuwalea katika maadili mema ya Kikristo, na kuwasaidia kuwa mashahidi wa Kristo katika maisha yao ya kila siku.
Karibu watoto wote kujifunza na kukuza imani yao kupitia Shule ya Jumapili!