huduma ya kichungaji
Huduma za Kichungaji Nje Ya Kanisa
Huduma za Kichungaji Nje ya Kanisa katika Kanisa la KKKT hubadilika kulingana na mahitaji ya waumini na jamii husika. Huduma hizi zinahusisha kuwafikia waumini walioko majumbani, mahospitalini, kazini au maeneo mengine kwa lengo la kuwahudumia kiroho na kuwafariji.
Lengo kuu ni kuimarisha imani, kuleta faraja na kuonesha upendo wa Kristo kwa wale wasioweza kufika kanisani kutokana na sababu mbalimbali. Tunahamasisha waumini kutoa taarifa za mahitaji ili kuwezesha ufanisi wa huduma hizi.
Karibuni nyote kushiriki na kushirikisha wengine kwa ajili ya kujengwa kiroho!