Vikundi
UMOJA WA WAKINAMAMA
Umoja huu umeundwa na wanawake wote katika usharika.
Dira Yetu
Dhima ya kikundi hiki ni kuwa na umoja na mshikamano mkubwa kuweza kuwa mfano mzuri kwa wanaotuzunguka na kuwa na upendo popote tunapokuwa.
Malengo Yetu
Dira ya Umoja wa kina mama ni kuwa kikundi bora chenye kumjua MUNGU nakuwa na miradi yenye tija ya kuweza kusaidia wanawake na mabinti wenye uhitaji.
- SIFA ZA KUJIUNGA NA UMOJA WA WAKINAMAMA
- Awe amejiandikisha na ana namba ya ahadi n.k.
- Awe kwenye jumuiya zetu.
- Awe anashiriki meza ya Bwana
- Mcha Mungu
- Awe mama msharika
- KAZI MBALIMBALI ZA UMOJA WA WAKINAMAMA
- Kupokea wageni toka nje na ndani ya Dayosisi n.k.
- Kukutana na mabinti wenye kuhitaji huduma kutoka kwa wanawake wazee
- Kufanya usafi usharikani
- Kutembelea waliofiwa
- Kutembelea wagonjwa
- UONGOZI WA UMOJA WA WAKINAMAMA
| Cheo | Jina | Mawasiliano |
| Mwenyekiti | Merry John | 25578900000 |
| Katibu | Neema Joseph | 25578900000 |
| M/Mwenyekiti | Sarah Baraka | 25578900000 |
