Vikundi
UMOJA WA VIJANA
Ni Kumlea kijana kimwili, kiakili na kiroho.
Dira Yetu
Ni kuhakikisha tunafanya kazi ya kuwajenga Vijana katika kila Nyanja ya kiuchumi, kiroho na kiakili.
Malengo Yetu
Ni Kuona kijana amekua kimwili, kiuchumi, kiakili na kiroho.
- SIFA ZA KUJIUNGA NA UMOJA WA VIJANA
- Vijana wa usharika wa Kimara.
- Mkristo, Mlutheri aliyepata Kipaimara mwenye umri kati ya miaka 13 na 35.
- Mkristo, Mlutheri ambaye hajapata Kipaimara na mwenye umri zaidi ya miaka 35 anaruhusiwa kushiriki ila hatakuwa na haki ya kuchagua au kuchaguliwa kuwa kiongozi n.k.
- Mkristo wa dhehebu lingine anaruhusiwa kushiriki iwapo anakubaliana na taratibu na miongozo ya KKKT – DMP ila hatachaguliwa kuwa kiongozi.
- Atakayekuwa na kadi ya uanachama iliyotayarishwa na Idara ya Vijana ya KKKT – DMP ambayo atalipia kiingilio na ada ya kila mwezi.
- KAZI MBALIMBALI ZA UMOJA WA VIJANA
- Uimbaji kwa lengo la kupamba Ibada, Mikutano, Sherehe mbalimbali, mahubiri na kutoa faraja kwa wagonjwa na misiba.
- Sanaa mbalimbali za maonesho na za mikono kama vile Maigizo, Ngonjera, Mashairi, vichekesho, Majigambo, uchoraji, uchongaji, ufumaji, ufinyanzi n.k.
- Kuweka utaratibu wa mafundisho ya Biblia na masomo mbalimbali kwa vijana.
- Kucheza michezo ya nje na ya ndani.
- Kuanzisha na kuendesha miradi halali ya kiuchumi.
- UONGOZI WA UMOJA WA VIJANA
Cheo | Jina | Mawasiliano |
Mwenyekiti | John John | 25578900000 |
Katibu | James John | 25578900000 |
M/Mwenyekiti | Baraka Amani | 25578900000 |